Elimu juu ya Tetenasi (Tetanus)

Tetenasi ni ugonjwa unaosababishwa na bacteria wanaoitwa ( Clostridium tetani). Wadudu hawa wanapatikana katika mazingira yanayotuzunguka mfano; ardhi, misumari au vitu vyenye ncha, vinyesi vya baadhi ya wanyama nk. Bacteria wa tetenasi wanaweza kuishi katika mazingira kwa miaka mingi. Pia wanapenda vidonda, ndio maana wanaingia mwilini kupitia vidonda au mikwaruzo. Dalili za Tetenasi zinatokea siku 4-14 baada ya kupata jeraha. Tetenasi imegawanyika sehemu mbili. Tetenasi inayotokea kwa watu wazima (adult) Tetenasi ya watoto (neonates) Nani yupo hatarini kupata tetenasi? Kwa watu wazima (Adults) Ikiwa umeumia na kupata jeraha au kidonda sehemu ya mwili wako uko katika hatari ya kupata ugonjwa huu hatari wa tetenasi. Ikiwa umetobolewa na msumari una zaidi ya 32% kupata tetenasi. Ikiwa umeungua, au watu wanaojidunga sindano za madawa ya kulevya, au watu wanaojiwekea tattoo, watu wenye magonjwa ya meno, wapo katika hatari ya kupata ugonjwa...