Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia 2017

KAMA UNASUMBULIWA NA MAUMIVU YA KICHWA SOMA HAPA

Picha
Maumivu ya kichwa ni hali inayosumbua watu wengi kwa sasa, hii ni kutokana na kuongezeka kwa magonjwa ambayo yanakuja na dalili za kichwa kuuma, uchovu wa kila siku, hewa nzito ya carbon dioxide na kelele nyingi za viwandani na magari.  Baadhi ya magonjwa na tabia zinayosababisha kichwa kuuma ni kama zifuatazo.   1. Utumiaji wa madawa ya kulevya na pombe.   2. Magonjwa ya macho mfano  refractive errors   3. Magonjwa ya ubongo mfano i.e meningitis   4. Uvimbe ndani ya ubongo i.e brain tumour   5. Magonjwa ya mifupa ya usoni i.e sinusitis   6. Cervical degenerative osteoporosis i.e magonjwa ya mifupa ya uti wa mgongo   7. Magonjwa ya moyo i.e presha ya damu   8. Mgandamizo wa mawazo.  Matibabu ya kiasili   Kutibu chanzo yaani ugonjwa uliosababisha kichwa kuuma ndio njia bora ya kutibu maumivu ya kichwa.  Kama chanzo cha maumivu ya kichwa hayafahamiki njia zifuatazo zina...

MAUMIVU YA TUMBO

Picha
Maumivu ya tumbo ni dalili inayosumbua watu wengi kwa wakati na umri tofauti. Karibu kila mtu katika maisha yake atapata namna fulani ya maumivu ya tumbo. Kuna sababu mbalimbali zinazosababisha maumivu ya tumbo na mara nyingi huwa sio za kutisha, hutubiwa na kupona. Mara chache husababishwa na hali ambazo zinaweza kuhatarisha maisha yako. Maumivu yanaweza kuwa katika sehemu maalum ya tumbo au tumbo zima.  Maumivu Ya Tumbo   Ni vizuri ukijua aina ya maumivu ya tumbo unayopata pamoja na dalili zinazoambatana nayo. Hii itasaidia kujua sababu ya maumivu na katika matibabu. Maumivu ya tumbo yanaweza kuwa maumivu ya kuchoma, kuungua, kukandamiza, kukata au. Yanaweza kuwa yanakuja na kuacha baada ya muda fulani. Pia yanaweza kuambata na dalili nyingine kama kutapika, kuharisha, kukosa choo, kupata choo chenye damu, tumbo kuvimba na homa.  Sababu za Maumivu ya Tumbo   Kuna hali nyingi zinazoweza kusababisha maumivu ya tumbo. Chanzo cha maumivu hutegemea na sehemu maumiv...

BIZARI: KIUNGO CHA MBOGA CHENYE FAIDA NYINGI

Picha
Inawezekana katika maisha yako hujawahi kula mboga iliyowekwa kiungo kinachoitwa bizari, kama umewahi, inawezekana pia hujawahi kujua faida zake mwilini.  Bizari (Turmeric) ni kiungo cha mboga jamii ya mimea unaochimbwa kama mizizi, mfano wa tangawizi, lakini tangawizi yenyewe ina rangi ya njano na hujulikana pia kama ‘manjano’ kutokana na rangi yake.  Kiungo hiki kinatumiwa sana katika Bara la Asia na hasa India na China. Kutokana na umuhimu wake kiafya, vyakula vingi hupikwa kwa kuchanganya na kiungo hiki ambacho sasa kimeenea dunia nzima, ikiwemo Tanzania.  FAIDA ZA BIZARI KIAFYA   Bizari hutumika na watu wengi kama kiungo cha mboga cha kuongeza ladha katika mchuzi na pengine kuweka rangi, lakini kuna faida nyingi unazozipata unapotumia kiungo hiki kila mara katika mapishi yako.  Inaelezwa kuwa bizari ina virutubisho vyenye uwezo wa kuimarisha kinga ya mwili, mara 8 zaidi ya Vitamin C na Vitamin E, ina uwezo wa kushusha kiwango cha lehemu (cholesterol) ...

Dalili za Ugonjwa wa zinaa - kisonono

Picha
Kisonono ni ugonjwa wa zinaa unaoambukizwa, ugonjwa huu hutokana na wadudu aina ya Neisseria gonorrhoeae. Ugonjwa huu pia huambukizwa kwa tendo la ngono na hata kutoka kwa mama mjamzito anapojifungua huweza kumuambukiza pia mtoto endapo atakuwa alikuwa nao.  Ugonjwa wa kisonono kwa mara nyingi huwapata vijana na watu wazima. Waathirika wengi wa ugonjwa huu wa kisonono huambatana na magonjwa mengine ya zinaa, kwasababu kunabaadhi ya magonjwa mengine ya zinaa hujificha bila kuonyesha dalili, hivyo kukuta ukiugulia ndani kwa ndani.  Ugonjwa wa kisonono, unazuilika na kutibika pia, unaposikia dalili zozote za magonjwa ya zinaa, unashauriwa kumchukua mwenzi wakona kuwahi hospitali  kuchukua vipimo kwaajili ya matibabu.  DALILI ZA UGONJWA WA KISONONO.   Mara nyingi ugonjwa wa kisosnono huwa hauonyeshi dalili yoyote mwanzoni. Lakini ukionyesha dalili basi kwa mwanaume utasikia maumivu makali wakati wa kukojoa na kuambatana na usaha kutoka uumeni, kwa mwanamke pia ...

Vyakula Hatari kwa Kupunguza Nguvu za Kiume

Picha
Mbegu za Flax (Flax seeds):     Wanaume wanapaswa kufahamu aina ya vyakula ambavyo si rafiki kwao katika kuongeza kiwango cha homoni ya kiume iitwayo testosterone inayochochea sifa ya mwanaume yaani kuwa na nguvu za kiume. Baadhi ya vyakula visivyofaa kuliwa na mwanaume aliyetaka kuwa na nguvu za kiume ni vile vyenye asili ya homoni ya kike iitwayo estrogen. Hivyo sio kila vyakula vinafaa kwa mwanaume eti ilimradi tu vyakula hivyo vinasaidia kujenga mwili au kujaza tumbo wakati mtu akiwa na njaa.  Vyakula visivyofaa kabisa kuliwa na mwanaume kutokana na vyakula hivyo kupunguza homoni ya testosterone ni hivi vifuatavyo:  vyakula vinavyotengenezwa kutokana na unga wa mbegu za flax vimekuwa vikisifiwa kwa kuwa Omega-3 fats ambayo ni muhimu katika miili yetu. Hata hivyo mbegu za flax ni mbegu maarufu kwa kuwa na estrogen ambayo ni sawa kabisa na homoni ya estrogen iliyoko katika miili ya wanawake.  Flax seeds zina kiwango cha phytoestrogens mara tatu zaidi...

Maradhi Yanayotibiwa na Habbat Soda (BLACK SEEDS)

Picha
Yafuatayo hapa chini ni baadhi ya matatizo na magonjwa ambayo yanaweza kutibika kwa kirahisi kwa kutumia Habbat-Sawdaa.  Vipele (chunusi) Na Ngozi:    Changanya na pasha moto kwa dakika mbili kikombe kimoja cha Habbat-Sawdaa iliyosagwa, ½ (nusu) kikombe cha maganda ya komamanga yaliyosagwa, na ½ (nusu) kikombe cha siki ambayo inatokana na juisi ya tofaha (apple). Paka katika sehemu inayotakiwa kabla ya kwenda kulala kila usiku mpaka vipele (chunusi) vitakapoondoka. Mchanganyiko unaweza kukaa mpaka wiki tatu na ni lazima uwekwe katika hali ya ubaridi.  Upara (Alopeshia):    Sugua mafuta ya Habbat-Sawdaa katika mabaka yanayokusumuba.  Pumu:    Tia ½ (nusu) kijiko cha Habbat-Sawdaa iliyochemshwa katika maji ya yaliyochemshwa kisha unywe moto.  Kuumwa kwa Mgongo (Sehemu ya Chini):    Changanya asali pamoja na ¼ (robo) kijiko cha Habbat-Sawdaa na iwe kitu cha kwanza kunywa wakati wa asubuhi kabla ya kufu...

Kifafa cha Mimba (Preeclampsia, eclampsia)

Picha
Kifafa cha mimba ni ugonjwa unaohusiana na msukumo mkubwa wa damu (high blood pressure) wakati wa ujauzito pamoja na kuharibika kwa viungo muhimu mwilini kama vile figo na ini. Kwa kawaida ugonjwa huu hutokea baada ya nusu ya kwanza ya ujauzito kuisha (kuanzia wiki ya 20 au miezi mitano ya ujauzito).  Ugonjwa huu huweza kuwatokea hata wajawazito ambao hawakuwa na tatizo la msukumo mkubwa wa damu kabla ya ujauzito.  Ugonjwa wa kifafa cha mimba unaweza kuleta madhara makubwa kwa mjamzito na mtoto aliye tumboni. Kuharibika kwa viungo muhimu kama figo na ini la mjamzito kunaweza kuwa kwa kiwango kikubwa kichoweza kusababisha mjamzito kupoteza maisha iwapo hatapata huduma ya afya mapema. Vilevile mtoto aliye tumboni anaweza kuathirika kwa kukosa damu ya kutosha toka kwa mama na kushindwa kukua vizuri na iwapo hali hiyo ikiendelea muda mrefu anaweza kufia tumboni.  Kutokana na hatari kubwa ya ugonjwa huu kwa wajawazito na watoto walio tumboni, inashauriwa kila mjamzito awe ...

USHAURI MUHIMU UKIWA UKO PEKE YAKO NJIANI NA UMEPATWA NA SHAMBULIA LA MOYO (HEART ATTACK) CHUKUWA TAHADHARI. 

Picha
Chukulia ni muda wa saa 1:25 usiku unarudi nyumbani peke yako, baada ya kazi ngumu zusizo za kawaida ofisini.Umechoka sana, una hasira na umechanganikiwa.Ghafla unajisikia maumivu makali kifuani yanaelekea mkononi na hata kwenye Taya. Upo umbali wa kama km5 tu kufika Hospitali iliyo karibu na kwako.Bahati mbaya hujui kama utaweza kufika kwa vunavyojisikia.Ulishafundishwa kumfanyia mtu CPR, lkn aliyekufundisha hakuwaambia unaweza kujifanyia mwenyewe. JINSI YA KIJUSAIDIA UNAPOPATWA NA SHAMBULIO LA MOYO UKIWA PEKE YAKO . Kwa kuwa watu wengi hupatwa na Shambulio la Moyo wakiwa peke yao bila msaada wowote, mtu ambaye mapigo yake ya Moyo hayako sawa na anaanza kuhisi kuzimia, au zimebaki sekunde 10 tu kabla hajapoteza fahamu.Hata hivyo, waathirika hawa wanaweza kujisaidia kwa kujikoholesha mfululizo. Avute pumzi ndefu kila unapo jikoholesha, na kikohozi lazima kiwe cha ndani mfululizo mpaka makohozi yatoke ndani ya kifua.Kikohozi hicho kiendelee mpaka utakapopata msaada au mpaka mapigo y...

Figo Kushindwa Kufanya Kazi (Renal/Kidney Failure)

Picha
Figo ni miongoni mwa viungo muhimu sana katika mfumo wa utendaji kazi wa mwili wa binadamu. Kwa kawaida, mwili wa binadamu una figo mbili zenye maumbo yanayofanana kama yale ya maharage, yakiwa yamejificha nje ya utando unaozunguka tumbo, chini kidogo ya mbavu za chini.  Kazi za figo   Kazi kuu za figo ni kuchuja vitu mbalimbali pamoja na sumu kadhaa katika damu na hivyo kusaidia katika kuhifadhi na kuthibiti kiwango cha maji na madini (electrolytes) mwilini. Katika kutekeleza hayo, figo huchuja vitu hivyo pamoja na maji yaliyo mwilini na kutengeneza mkojo, huchuja pia maji yasiyohitajika mwilini huku yakinyonya madini na kemikali muhimu kuzirudisha katika mzunguko wa damu na kutoa nje uchafu usiohitajika.  Kazi nyingine za mafigo ni   Kurekebisha na kuthibiti kiasi cha vitu mbalimbali katika damu pamoja na kiasi cha maji katika mwiliHusaidia kutengeneza kiasili cha erythropoietin ambacho ni muhimu sana katika utengenezaji wa chembe nyekundu za damu.Husaidia uza...

Ugonjwa Wa Kukojoa Damu (Haematuria)

Picha
HAEMATURIA ni ugonjwa wa kukojoa damu ambapo kwenye mkojo kunakuwepo chembechembe za damu nyekundu (Red blood cells).  Kukojoa damu ni dalili ya kuonyesha kuwa mtu anayekojoa ana magonjwa katika mfumo wa mkojo kama vile magonjwa ya kichocho au magonjwa mengine yanayoshambulia kibofu cha mkojo au kwenye figo.  SABABU   Magonjwa yanayoshambulia mfumo wa mkojo kama vile UTI, magonjwa ya zinaa hasa kwa wanawake, vijidudu kama staphylococcus saprophyticus, mawe kwenye figo (kidney stone) kuvimba kwa tezi zinazozalisha manii kwa wanaume ambao umri  umeenda yaani wazee.  Sababu nyingine ni kama kupata ajali na kuumia sehemu za mfumo wa mkojo (trauma), kupata magonjwa kama kansa  ya kibofu cha mkojo, hii hutokea  mara nyingi hasa  vijijini  ambapo watu wanacheza au kuogelea kwenye madimbwi ya maji yasiyotembea.  Sababu zingine  ni mtu kuugua magonjwa ya sickle cell anemia na magonjwa mengine  ya figo kama vile nephotic syndrome n...

Shambulizi La Moyo "heart attack"

Picha
Moja ya magonjwa hatari sana ambayo yanaweza kumpata mtu yoyote ni ugonjwa wa shambulizi la moyo. Huu ni miongoni mwa magonjwa yanayoongoza kwa kusababisha vifo vya wanaume na wanawake.  Kwa kawaida, ugonjwa huu hutokea pale ambapo sehemu ya nyama ya moyo inapoharibika au kufa kutokana na kukosa damu ya kutosha.  Je tatizo hili husababishwa na nini?Husababishwa na kuziba kwa mishipa ya damu inayosambaza damu katika moyo (coronary artery blockage) kutokana na mafuta mabaya mwilini (atherosclerotic plaque).  Watu gani wapo katika hatari ya tatizo hili?Watu walio katika hatari ya kukumbwa na ugonjwa huu ni pamoja na  Wenye umri mkubwa miaka 45 kwa wanaume na 55 kwa wanawakeWavutaji wa sigaraWatu wenye mafuta ya lijamu katika damu au wale wenye mafuta mabaya aina ya triglycerides na low density lipoprotein kwa kiwango kikubwa katika damu zaoWenye kisukariWenye matatizo ya shinikizo la damuWalio na unene kupita kiasi (obesity)Wenye matatizo sugu ya kushindwa kufanya ...

Dalili Ya Kuzidi Asidi Mwilini na tiba yake!

Picha
DALILI YA KUZIDI ASIDI MWILINI:  ONYO: Mwanamke Mwenye mimba asinywe hii dawa Tafadahali sana.  Sababu ya Acidity   • Uvutaji wa sigara kwa wingi  • Kunywa pombe kupita kiasi  • Vidonda vya tumbo  • kuzidi kwa asidi ya tumbo  • Kutokula kwa wakati  • Kula kukaanga na viungo vya chakula mara kwa mara  • Matatizo katika utendaji wa mfumo wa mmeng'enyo wa chakula tumboni  • Kukaa na njaa kwa muda mrefu au kuto kula chakula cha Asubuhi  • Kula vyakula vingi vya mafuta, kama chocolates  • kuwa na Mimba kunasababisha asidi pia.  • kuzeeka  • Utokaji yatokanayo na jua na joto  • Muafaka wa chakula tabia  • kuwa hisia mbaya  • Udhaifu wa mishipa ya mwilini  Dalili ya Acidity   • Mchomo au maumivu katika tumbo, 1-4 masaa baada ya mlo  • maumivu ya kifua  • Kiungulia cha Muda mrefu  • Uvimbe katika kifua  • Kuhisi njaa mara kwa mara  • Daima maumivu kati...

Sababu Tisa (9) Za Kiafya Kwanini Unatakiwa Kutumia Zabibu Kila Wakati

Picha
Kwa mujibu wa tafiti za kiafya zinaonyesha, ipo faida kubwa sana kwa mtu yeyote anayetumia zabibu katika upande wa afya yake.  Inaonyesha moja kwa moja, zabibu kutokana na wingi wa madini zilizonayo ndani yake, zina uwezo wa kutibu magonjwa mbalimbali kama zikitumiwa kwa uhakika. katika makala haya tumekuwekea dondoo za kukusaidia kukuonyesha baadhi ya magonjwa yanaweza kutibiwa au kuepukwa hasa kutokana na matumizi ya zabibu.  1. Zabibu inatibu pumu (Asthma)  2. Zabibu ina imarisha mifupa.  3. Zabibu inazuia magonjwa mengi ya moyo.  4. Zabibu inapunguza unene kwa sehemu.  5. Zabibu inapunguza kisukari.  6. Zabibu ni kinga ya magonjwa ya meno.  7. Zabibu ni kinga kwa kansa ya matiti.  8. Zabibu inapunguza ugonjwa wa mapafu.  9. Zabibu inapunguza tatizo la kushindwa kuona mbali.

Afya zetu kwa parachichi

Tumezoea kupaka parachichi directly katika ngozi, lakini pia kula parachichi kuna faida nyingi katika ngozi na mwili wako, parachichi zina sifika kwa kuwa narich healthy fatty acids, vitamins na antioxidants ambazo zina weza ku improve ngozi yako kwa ndani. Hizi ndizo Faida 5 za parachichi Huipa ngozi unyevu  –Ni nzuri sana kwa ajili ya kutibu ngozi kavu sana na ngozi iliyo zeeka.  mafuta ya parachichi  yana uwezo wa ajabu wa ku moisturize ngozi yako na kuipa muonekano mzuri unacho takiwa kufanya ni kabla ya kulala chukua matone ya mafuta ya parachichi paka katika ngozi fanya hivi kila siku na utaona matokeo ndani ya siku chache  Husaidia  Kupambana na uzee   – Avocado ni tiba ya ajabu ambayo husaidia kupunguza mikunjo ya uzee. Si tu unaweza kupaka parachichi  mwilini na katika ngozi yako kama mask, lakini pia kula avocado husaidia kupambana na kuzeeka  kutoka ndani. Kila mwanamke anataka kuweka ngozi yake katika hali  ya ujana na kuo...

MBOGA MAJANI NA FAIDA ZAKE

MBOGA ZA MAJANI Watu wana mtazamo tofauti kwamba vyakula vyenye virutubisho kwa kawaida hutumia bei ghali kati ya aina ya vyakula.Wanasahau kwamba mazoea pia hutuwekea uwazi na aina za vyakula ambavyo vina virutubisho na vinaweza kununuliwa kwa kiasi cha chini.Wapo wenye vikwazo vya kutumia mboga za majani,Mara nyingi watu wana athiriwa na desturi ya vyakula kama mwiko kwao kuvila na kuweka imani kuwa hakuna ujuzui wa kisayansi uliohusika.Hii ipo mbali zaidi utatanishi wa watu ambao wameubeba nje na hadhi ya manufaa yanayohusika kwenye chakula na kutokumbukwa thamani ya virutubisho vyake.Kwa mfano,ni kawaida kuwa na imani mboga za majani ya kijani ni chakula cha watu masikini na hazina hadhi ya kutumiwa.Ni kweli kwamba mboga za majani sio ghali sana, hii haiwafanyi kwa njia yoyote watu wa hali duni kukosa faida ya virutubisho. Ngoja tuangalie hizi mboga za majani kwa mtazamo tofauti,mtazamo wa virutubisho,Baada ya yote,mboga za majani zinatoa nini?Mboga za majani zote zina kitu ki...